Yapo mambo kadha wa kadha ambayo tungependa watumiaji wa lugha ya Kiswahili wayapate kupitia mitandao yao ya kijamii hasa kwa njia ya Twitter na blogu yetu hii ya #ElimikaWikiendi. Jambo kubwa katika yote yafanyikayo kupitia #ElimikaWikiendi ni kutoa Elimu mbalimbali kwa jamii ya wazungumza Kiswahili. Tunaamini kwamba, Elimu bora haipatikani darasani pekee bali hukamilika kwa kujifunza nje ya Darasa. Watu wengi wangetamani kujifunza mambo mbalimbali hasa kwa kupitia lugha ya Kiswahili, lakini tatizo ni kwamba watajifunzia wapi? Huu ndio mpango wetu #ElimikaWikiendi, kuwa Zaidi ya Darasa kwenye kubadilisha maisha ya watu kwa kutumia lugha yao waliyoizoea na kuizungumza kila iitwapo leo.
Je, ungetamanii kuwa mmoja wa waelimishaji kupitia #ElimikaWikiendi? Huu ndo mpangilio wa huduma zetu;
  • Kuwa mshiriki wa kila Jumamosi (ifikapo saa mbili asubuhi hadi saa nane mchana), kupitia 'twitter account' yako utaweza kusiriki midahalo yote itakayokuwa ikiendelea kupitia 'Twitter' kwenye neno #ElimikaWikiendi bure kabisa bila malipo yoyote na bila kizio cha namba ya jumbe zako.
  • Waweza kuwa mtoa mada kama mtu binafsi, shirika ama kampuni n.k. Kupitia #ElimikaWikiendi utapewa masaa maalumu ya kuendesha mada yako na mada hiyo itajadiliwa na wadau wote wa Kiswahili watakaofatilia #ElimikaWikiendi. Kutokana na wingi wa maombi ya wahusika kupewa kipindi tumeona ni vyema kuwe na uchangiaji wa kiasi kidogo cha fedha (Wasiliana nasi kujua zaidi).
  • Waweza kuwa mzungumzaji katika Blogu yetu ya #ElimikaWikiendi. Hii ni bure kwa watu wote. Jambo la muhimu ni kuwasiliana nasi na kutuma makala yako kupitia barua pepe, nasi tutakuwa tunairusha makala yako. Hii iko wazi kwa kila mtu kutoa makala yake anayoipenda kwa lugha ya Kiswahili.
  • Waweza kujitangaza kupitia Blogu yetu kwa bei nafuu kabisa (Wasiliana nasi kwa maelezo zaidi)
Muhimu;  #ElimikaWikiendi haizungumzii siasa, bali habari zote zenye kuelimisha Jamii ya            wanaokizungumza Kiswahili. Lugha yetu ni moja tu, nayo ni KISWAHILI PEKEE!!!

0 comments:

Post a Comment

Kutoka Twitter

Zilizo Maarufu

Tangaza Nasi

Tangaza Nasi

Tuachie Ujumbe