Na Dr.
Sajjad Fazel (PharmD.)
Mtaalamu wa Madawa na Tiba
Shisha
ni uvutaji wa tumbaku uliochanganywa na ladha za matunda mbali mbali kwa
kutumia hookah. Hookah ni chombo kinachohifadhi maji na huwa ina mirija kuanzia
eneo lakuchoma tumbaku kupitia maji mpaka mirija yakuvutia moshi mdomoni.
Shisha
ni kitendo cha burudani iliyoenea nafasi nyingi hapa Tanzania mpaka imekua kitu
cha kawaida. Burudani hii siyo tabia ya waafrika ki asili bali ni tabia ya
warabu. Warabu huvuta shisha kwasababu ipo ndani ya mila yao. Watu wengi
Tanzania wameiga tabia hiyo bila kujua madhara yake.
Uvutaji
wa shisha inamadhara mengi kuliko uvutaji wa sigara. Hii ni kwasababu ya muda
na idadi ya moshi unaovutwa. Mtu anayevuta sigara huwa anavuta mililita 30 ya
moshi mara ishirini. Lakini mtu anayevuta shisha kwa saa moja, huwa anavuta
mililita 500 ya moshi mara 200. Kwa ujumla anayevuta sigara anavuta takriban
mililita 600 ya moshi wakati anayevuta shisha anavuta mililita 100,000 ya moshi
kwa ujumla. Hivyo, mvutaji wa shisha huvuta moshi wa idadi ya sigara 100.
Madhara
ya shisha hutokana na madhara yanayosababishwa na tumbaku. Tumbaku husababisha
saratani aina 20, ikiwemo saratani ya mapafu, mdomo, koo, figo, kongosho, ini,
tumbo na kadhalika. Tumbaku inayo chemikali sumu zinazosababisha saratani.
Pamoja na hilo Chemikali sumu ndani ya tumbaku husababisha tatizo la moyo,
tatizo la ufizi wa meno, kupunguza nguvu zakiume na tatizo la mapafu kwa
ujumla.
Watu
wengi wakivuta shisha, huwa wanatumia hookah moja. Tatizo lakutumia hookah moja
ni mambukizi ya magonjwa. Kwa mfano; kama mtu moja anayo tatizo la kifua kikuu
au kisamayu, kwa kutumia hookah ule ule anaweza kuwaambukiza wenzie.
Wakina
dada pia wanapenda kujihusisha na mambo ya shisha. Ni muhimu kwa wale waliokuwa
wajawazito waelewe kwamba uvutaji wa shisha huleta madhara kwa mtoto tumboni. Watoto
wanaozaliwa kwa wale wanaotumia shisha huwa wanatatizo la mapafu pamoja na
uzito mdogo sana.
Tumbaku
pia huwa inayo nikotini. Nikotini inasababisha mazoea kwa wavutaji sigara na
shisha. Nikotini ndicho kinachofanya mwili ipate mvutio na tumbaku (addiction).
Ni vizuri watu waelewe tatizo la kuzoea shisha na ugumu wakuiacha baada
yakutengeneza mazoea.
Kuna
fikra moja la uwongo kwamba moshi ya shisha Ikipita ndani ya maji, huwa yanatoa
chemikali sumu zinazosababisha saratani na nikotini. Huo si kweli. Utafiti zinaonyesha
maji hayaondoi chemikali sumu inayopatikana ndani ya tumbaku.
Kama
mtu yeyote anayo maswali, anaweza kuniuliza.
Asante.
Facebook; Dr. Sajjad Faze
Twitter; Dr. Sajjad Fazel @SajjadF
Instagram; Afya Yako @afyatz
Makala ni nzuri na inaelimisha jamii kwakweli!hongera sana mkuu
ReplyDeleteAsante Mkuu
Delete