Monday, 4 July 2016


Mara kadhaa, wazazi au walezi huwataka watoto wao wajifunze lugha ya ziada au nyingi ili tu wawe wa tofauti au kuwafikiria hapo baadaye kwenye maswala ya ajira. Lakini leo nimekuletea sababu sita za msingi kwanini wewe kama mtu mzima unatakiwa ujifunze lugha au kama mzazi unatakiwa kuhakikisha mtoto wako anajifunza lugha nyingi kadiri iwezekanavyo;

1. Huongeza nguvu ya ubongo
Kujifunza lugha nyingi huongeza uwezo wa ubongo wako kufikiri maradufu. Ni njia nzuri ya kufanya ubongo wako uwe na afya na sharp muda wote. Tafiti zinaonesha kuwa, watu wanaofahamu lugha nyingi huwa vizuri katika kuchakata lugha na maswala mengine ya kiuchambuzi. Kuweza kubadilisha kutoka lugha moja hadi nyingine husababisha sehemu ya ubongo wako inayohusika na utatuzi wa mambo na mchujo wa taarifa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Pia, ubongo ambao upo active husaidia kupunguza hatari za kupata magonjwa ya nyuroni kama vile dimetia.

2. Lugha ni geti la kuingia na kufahamu tamaduni nyingine
Lugha ni moja kati ya njia nzuri zaidi ya kujifunza kuhusu utamaduni mpya. Ukifahamu lugha fulani, itakufanya moja kwa moja uwe na shauku ya kufahamu kuhusu utamaduni fulani kwasababu mara nyingi, kufasiri jambo fulani kutoka katika lugha nyingine ili lieleweke katika lugha lengwa hushindwa kubeba maudhui yote yaliyokusudiwa katika muktadha wa jambo husika.

3. Utakuwa na uwezo wa kuwasiliana katika lugha nyingine
Kujifunza lugha nyingine hukulazimisha kuboresha uwezo wako wa kusikiliza na kuelewa na pia kukusaidia kuangalia lugha yako ya awali katika upande wa pili. Pia kujifunza lugha ya pili husaidia  uweze kupata michongo na watu wengi zaidi na itakufanya uwe sehemu ya jamii inayozungumza lugha hiyo.

4.  Inafanya kusafiri kwako kuwe rahisi na kufurahia
Kama unataka kuwa mtu anayesafiri kwenda sehemu mbalimbali duniani, basi kujifunza lugha ni jambo muhimu. Kusafiri ni njia ya kufurahia uzuri wa dunia na kujifunza mambo mapya, na kufahamu lugha fulani huondoa kikwazo katika kufanya hayo. Uwapo ugenini, hautohofia kuzurura hapa na pal3 kwasababu hauwezi kuwasiliana kirahisi,kwasababu utaweza kuzungumza na wenyeji bila kutegemea msaada wa vitabu vya utafsiri, lakini cha muhimu zaidi utajua chakula gani cha kuagiza bila ulazima wa kunyooshea kidole kwenye picha :)

5.  Inakufanya Kuwa Open-Minded na kuondoa utofauti wa kitamaduni
Sababu kubwa ya ubaguzi wa kitamaduni na rangi ni kukosa uelewa kuhusu watu mbalimbali na utofauti katika tamaduni zao. Kufahamu lugha hutoa fursa pana ya kujifunza kuhusu wahusika wa lugha hiyo na tamaduni zao lakini pia husaidia wewe kuheshimu tamaduni za wengine. Muhimu pia, husaidia kuleta mshikamano, uvumilivu wa utamaduni na uelwa hasa katika mambo yanayohitaji ushirikiano kati ya watu tofauti ili kuyafanikisha.

6. Itakufanya uwe raia bora wa kidunia (Global Citizen)
Kama bado hujashitukia dili, faida na fursa zote zinazikuja na kujifunza lugha nyingi zitakufanya uwe raia bora wa dunia, Utajisikia na miguvu kila sehemu uwapo.

Yapo mambo mengi ambayo ningependa tuzidi kuyajadili kupitia jamvi la #ElimikaWikiendi, hivyo nakuomba tuzidi kuwa pamoja.

Mwandishi & Mtunzi,

Kennedy Daima Mmary

Saturday, 2 July 2016

Na Dr. Sajjad Fazel (PharmD.)
Mtaalamu wa Madawa na Tiba

Shisha ni uvutaji wa tumbaku uliochanganywa na ladha za matunda mbali mbali kwa kutumia hookah. Hookah ni chombo kinachohifadhi maji na huwa ina mirija kuanzia eneo lakuchoma tumbaku kupitia maji mpaka mirija yakuvutia moshi mdomoni.
Shisha ni kitendo cha burudani iliyoenea nafasi nyingi hapa Tanzania mpaka imekua kitu cha kawaida. Burudani hii siyo tabia ya waafrika ki asili bali ni tabia ya warabu. Warabu huvuta shisha kwasababu ipo ndani ya mila yao. Watu wengi Tanzania wameiga tabia hiyo bila kujua madhara yake.

Uvutaji wa shisha inamadhara mengi kuliko uvutaji wa sigara. Hii ni kwasababu ya muda na idadi ya moshi unaovutwa. Mtu anayevuta sigara huwa anavuta mililita 30 ya moshi mara ishirini. Lakini mtu anayevuta shisha kwa saa moja, huwa anavuta mililita 500 ya moshi mara 200. Kwa ujumla anayevuta sigara anavuta takriban mililita 600 ya moshi wakati anayevuta shisha anavuta mililita 100,000 ya moshi kwa ujumla. Hivyo, mvutaji wa shisha huvuta moshi wa idadi ya sigara 100.

Wednesday, 29 June 2016


Baada ya ukoloni kuisha afrika, jamii zetu zilianza kujitegemea kwa kila kitu; shughuli za kibiashara, siasa na kijamii (tamaduni, mila na desturi). Kila jamii ilikua na njia zake za kulea watoto na kwa asilimia kubwa zilikua zikilingana. Wazee walilea watoto wao na kuwarithisha malezi ambayo watoto waliweza kuwalea watoto wao sawa na walivyolelewa. 

Ni hadithi tulizo pata kutoka kwa wazazi wetu na bibi na babu zetu. Wanaume ndio walikua na sauti katika jamii, katika familia baba ndiye aliyekua na sauti na maamuzi juu ya familia, mlezi mkuu alikua ni mama kwani muda mwingi alikua na watoto, mara nyingi ushauri na tabia za watoto alikua akijua mama. Watoto hawakua na uwezo wa kutoa ushauri katika familia, ni mama na baba ndio wenye kauli na ushauri. Watoto walikua wakirithishwa malezi, tamaduni, mila na desturi kwa vitendo na maneno. Jinsi ya kuishi na watu, heshima na unyenyekevu kwa wakubwa na rika zao. 
Waazazi walikua wakiwafundisha shughuli za kufanya kwa vitendo na ukaribu; kulima, kuwinda, kufuga, kupika kwa ustadi mkubwa sana. 
Mtoto/kijana hakuwa na nafasi kubwa ya kujiamulia katika maisha yake, kwani alichaguliwa mke/mume wa kuoa au kuolewa nae. Mtoto alikuwa akichaguliwa na wazazi wake nini cha kusoma, nini cha kufanya kwa manufaa ya maisha yake ya baadae. Maisha ya watoto kwa asilimia kubwa yalikua chini ya uangalizi wa wzazi.
Imeandaliwa na:  Jalilu Zaidi;

                      Barua Pepe: jaliluzaid@gmail.com 
                      WhatsApp: +255656587011.

Habari ndugu msomaji na Mtanzania mwenye uzalendo na Taifa lake na mwenye dhamira ya wazi kabisa kuona kila kitu kinachomilikiwa na Tanzania kinaweza kupiga hatua na kusonga mbele zaidi ikiwemo Michezo, Muziki, Elimu, Nidhamu, Usalama, Amani, Demokrasia, Miundombinu, Lugha ya Taifa pamoja na mambo mengine mengi yanayopatikana kwenye Nchi yetu tuipendayo ya Tanzania. Kwanza kabisa nianze na maneno ya   Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage  Nyerere ambae  ametuasa tusiwe wabinafsi katika masuala yahusuyo taifa.   Suala la ubinafsi amelipiga vita tangu alipoasisi taifa hili na kutuagiza tuondokane na ubinafsi kama alivyoandika katika kitabu chake cha ‘Tujisahihishe.’ Kitabu hiki kilichapishwa mwezi wa  Juni ya mwaka wa  1962. Kwa maana hiyo, alitupa fursa ya kuielimisha jamii bila uchoyo na husuda kupitia njia mbali mbali ikiwemo Mikutano ya hadhara, Semina na Mikusanyiko ya Hadhara mbali mbali ili kuielimisha jamii ya Kitanzania. 
Njia nyingine raisi ambayo watu wengi tunaweza kujivunia sasa hivi kuna mitandao mingi ya kijamii ikiwemo tovuti mbali mbali Mfano;  jaliluzaid.com , chahali.com , millardayo.com , teknokona.com na nyingine nyingi  ambazo zinasaidia kwa kiasi kikubwa kuelimisha jamii na kuhabarisha pia jamii kwa lugha yetu ya Taifa ya Kiswahili maana kupitia kuhabarika jamii inapata kufahamu fursa mbali mbali za kimaendeleo hapa nchini na nje pia ya Nchi.

Monday, 20 June 2016

Kama ilivyo ada, #ElimikaWikiendi iko kwaajili ya kila mzungumza Kiswahili ili apate fursa ya kuelimika na kuwaelimisha wengine. Kuanzia sasa, matangazo yote ya vipindi vyote vitakavyokuwa vinakuja kupitia 'Twitter' ama matangazo ya kawaida kwako mzungumza Kiswahili yatakuwa yakiwekwa hapa. Usikose kupitia kila siku ili kuelimika zaidi na kuendelea kuwashirikisha ndugu, jamaa na marafiki ili nao waweze kuelimisha na kuelimishwa. Karibu sana, #ElimikaWikiendi ni zaidi ya Darasa!!!
                                                     







Kutoka Twitter

Zilizo Maarufu

Tangaza Nasi

Tangaza Nasi

Tuachie Ujumbe